Ombi la Bashe kwa kamati ya kuchunguza mchanga wa madini

0
168

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ameiomba Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar es Salaam, kurekori kilichomo katika makontena hayo ili yaoneshwe kwenye televisheni kwa lengo la kuwaondoa hofu Watanzania.

Ombi hilo limekuja siku chache baada ya Rais Magufuli kuunda Kamati kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

Alitoa ombi hilo bungeni mjini hapa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yaWaziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018.

Alisema wengi wanaamini kwamba yale makontena yaliyokamatwa bandarini yana dhahabu.

Alisema yeye ni miongoni mwa watu ambao wanaamini kwamba uwekezaji wa migodi mikubwa haujasaidia nchi ya Tanzania.

 

LEAVE A REPLY