Oliver Mtukudzi afariki dunia akiwa na miaka 66

0
133

Mwanamuziki wa Jazz Barani Afrika, Oliver Mtukudzi (66) ‘Tuku’ amefariki dunia katika Hospitali ya Avenues Clinic Jijini Harare nchini Zimbabwe leo Jumatano, Januari 23, 2019, jioni baada ya kuugua kwa zaidi ya mwezi mzima sasa.

Imeelezwa kuwa familia ya Mutukudzi inajipanga kutoa taarifa rasmi kuhusu kifo hicho, lakini vyombo vyote vya habri ikiwemo na mitandao ya kijamii nchini Zimbabwe imeripoti kifo hicho.

Mutukudzi ambaye alikuwa mbioni kuachia albamuyake ya 67 (Hanya’Ga), atakumbukwa kwa vibao vyake vingi vilivyotikisa Ulimwengu wa muziki, hasa wimbo wa ‘Neria’.

Oliver Mtukudzi (alizaliwa mnamo 22 Septemba 1952 mjini Highfield, Harare)  na ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.

Nyimbo ya kwanza ilikuwa “Dzandimomotera” iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki.

LEAVE A REPLY