Okwi aitosa Simba baada ya kujinga Sports Club Villa

0
383

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi amejiunga na klabu ya Sports Club Villa ya nchini Uganda.

Mshambuliaji huyo aliyeanza maisha yake ya soka kwenye klabu ya Sports Club Villa amerejea kwenye klabu hiyo kwa mkataba wa muda mfupi, ambao utamfanya achezee klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.

Okwi aliondoka SC Villa na kujiunga na Simba mwaka 2010 baada ya kuisaidia timu hiyo ya Uganda kushinda taji la nchi hiyo mwaka 2009.

Hata hivyo Simba bado inaweza kumpata mshambulaji huyo mwishoni mwa msimu huu kama hataamua kusaini mkataba mpya na klabu hiyo pindi mkataba wake wa sasa utakapomalizika na kama Simba bado itaendelea kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Kwa upande mwingine Hamsi Kiiza amejiunga na URA akitokea klabu ya Free State ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba, pia amesaini mkataba wa muda mfupi utakaomuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.

LEAVE A REPLY