Ofisi ya Makamo wa Rais kufadhili tathimini uaribufu mkoani Kagera

0
172

Ofisi ya Makamu wa Rais itafadhili kazi ya kutathimini uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu mjini Bukoba alipofanya ziara ya kikazi katika maeneo yaliyoathirika kwa tetemeko katika wilaya za Missenyi na Bukoba na kuuona hali ya uharibifu wa mazingira hayo.

Waziri Makamba, ameagiza mtaalamu mmoja kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kuungana na timu ya wataalamu walioko katika kituo cha Ihungo wanaofanya tathimini ya athari ya tetemeko ili kubaini mfumo gani uchukuliwe na serikali katika kuboresha miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu alisema, wameishaagiza wataalamu wapite katika kila eneo lililoathirika sambamba na taasisi za dini na shule za taasisi hizo ili kuona athari zilizotokea.

LEAVE A REPLY