Odinga na wenzake wameshindwa kutoa tangazo la mwelekeo wa chama chao

0
131

Muungano wa upinzani nchini Kenya, National Super Alliance (Nasa) umeahirisha kikao cha kutoa tangazo kuhusu mweleko wa chama hicho.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alikuwa ameahidi kwamba angetangaza ni hatua gani atachukua leo baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Ijumaa, ambapo mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.

Wakala mkuu wa Nasa Musali Mudavadi amesema sasa muungano huo unapanga kutoa tangazo kesho Jumatano.

Rais Kenyatta alitangazwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Hapo jana, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kususia kazi kabla ya kutoa tangazo kubwa leo.

Baada ya kutokea kwa maandamano katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na mji wa Kisumu, hali ya utulivu ilianza kurejea Jumatatu.

Viongozi wa muungano huo wa upinzani wanadai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba watu hao waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili.

LEAVE A REPLY