Nyumba za ibada kubomolewa leo Kimara

0
179

Nyumba za ibada 24 zinatarajiwa kubomolewa leo ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya.

Ubomoaji wa nyumba hizo za ibada ni mwendelezo wa uboamoaji wa nyumba takribani 1300 za wakazi wa maeneo hayo zinazodaiwa kujengwa ndani ya mita 121.5 ya barabara hiyo.

Ambapo nyumba zaidi ya 1000 zimebolewa mpaka sasa, amesema kwa siku ya leo kazi maalumu itakuwa ni kubomoa nyumba za ibada.

Aidha  shughuli za ubomoaji wa nyumba zimekamilika kwa asilimia kubwa ,zimesalia  nyumba za ibada tu.

Kazi ya ubomoaji itaanza mapema asubuhi ya leo kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya kwa ajili ya upanuaji wa Barabara hiyo.

LEAVE A REPLY