Nyoso akumbana na rungu la TFF

0
174

Shirikisho la Soka nchini, TFF limemfungia kutocheza mechi tano na faini ya shilingi milioni moja beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki.

Msemaji wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo amesema kuwa beki huyo amekutwa na adhabu hiyo kutokana na kitendo chake cha kumpiga shabiki baada ya kumalizika mchezo kati ya Kagera Sugar na Simba katika uwanja wa Kaitaba mijini Bukoba.

Ndimbo amesema kuwa kamati ya nidhamu ilimuita mchezaji huyo ambapo alikana kutenda kosa hilo badala yake alisema alimkunja tu lakini hakumpiga kabisa.

Kutokana na ripoti kutoka kwa mechi kamishna imeeleza kuwa Nyoso alimpiga shabiki huyo kwa kutumia kiatu na baadae akatumia goti kumpiga.

Nyoso si mara ya kwanza kufungiwa na shirikisho ilo kwani alishwahi kufungiwa kipindi akichezea klabu ya Mbeya City.

LEAVE A REPLY