Nyimbo za Alikiba na Ommy Dimpoz zapigwa Wasafi Tv

0
663

Baadhi ya mashabiki wa Bongo Fleva leo wameshangazwa baada ya kuona nyimbo za Alikiba na Ommy Dimpoz zikipigwa ndani ya Wasafi Tv inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Nyimbo za wasanii hao leo zimepigwa kwenye station hiyo licha ya kuwepo kwa tofauti kubwa kwa wasanii hao ambao ni mahasimu wakubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva mpaka kupelekea kuwa na makundi.

Kupitia akaunti ya Instagram ya mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kuwa Wasafi Tv ni Tv watu wote hivyo haitobagua msanii yoyote wa ndani.

Hapo hawali Diamond alisema kuwa anafungua Wasafi Tv kwa ajili ya kupromote muziki wa nyumbani na hatoangalia tofauti yoyote kwenye upigwaji wa nyimbo za msanii yoyote.

Alikiba na Diamond ni wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi ambao wamejizolea sifa kwa mashabiki wao kutokana na ubora wa kazi zao.

 

LEAVE A REPLY