Nyashinski afunguka kufanya kazi na Juma Jux

0
86

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Nyashinski ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Bebi Bebi’ amefunguka kwa kusema kwamba ana kolabo yake inakuja na muimbaji wa Tanzania, Jux.

Muimbaji huyo ameyasema hayo wiki hii wakati akizungumza na BBC kuhusu ujio wa kolabo zake na wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki.

Nyashinski amesema kwa Tanzania tayari amefanya kolabo na AY ambayo kwa sasa inapatikana katika mtandao wa YouTube.

Alisema kwasasa anatamani kufanya kazi na wasanii wa Uganda na Rwanda kwa kuwa bado hajafanya kazi na msanii wowote kutoka nchini.

Kuhusu kufanya kazi na wasanii wa WCB, msanii huyo amesema bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa label.

LEAVE A REPLY