Nuh Mziwanda akanusha kuwa na bifu na Diamond

0
792

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amefunguka na kudai kuwa hana bifu na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuaja baada ya watu kuhoji kutokuwa karibu na mwanamuziki huyo ambaye ni mmiliki wa lebo ya WCB.

Nuh ambaye ameshafanya ngoma na Ali Kiba aliomshirikisha katika wimbo wake wa Jike Shupa amefunguka na kusema hata kama hajawahi kufanya ngoma na Diamond haimaanishi wana bifu.

Kutokana na Bifu lililopo kati ya Diamond na Ali Kiba, wasanii wanaofanya kazi na wasanii hao hujikuta wakichagua upande wa kuwa na hivyo Mziwanda baada ya kufanya Kolabo na Ali Kiba alidaiwa kuwa na bifu na Diamond.

LEAVE A REPLY