Nuh Mziwanda afunguka mafanikio ya wimbo ‘Jike Shupa’

0
418

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amesema kuwa kolabo yake na mwanamuziki, Alikiba ‘Jike Shupa’ ilimuwezesha kuzunguka Tanzania nzima kwa ajili ya kufanya show.

Nuh Mziwanda amelazika kueleza hilo ikiwa ni jibu kwa wale waliokuwa wakisema nyumba aliyonesha kuwa ni yake haikuwa kweli.

Muimbaji huyo amesema fedha za ujenzi wa nyumba hiyo zilitoka kwenye tour alizokuwa akizifanya.

Amesema kuwa ‘Mimi sikuwa nafuatilia, kipindi kile ndio nilikuwa nimeachia Jike Shupa, nilifanya tour Tanzania nzima, chaka to chaka wilaya kwa wilaya,”.

Ngoma ya Jike Shupa ambayo ilitoka June 2016 ndio ngoma pekee kutoka kwa Nuh Mziwanda kufikisha views zaidi ya Milioni 2 katika mtandao wa YouTube.

LEAVE A REPLY