Nkurunzinza atangazwa kuwa kiongozi wa maisha chama tawala cha CNDD/FDD Burundi

0
72

Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.

Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

 

LEAVE A REPLY