Niva atabili mabaya mahusiano ya Harmonize na Kajala

0
60

Muigizaji wa Bongo Movie, Niva maarufu kama Super Mariyoo amefunguka na kusema kuwa mahusiano ya kimapenzi katika Harmonize na Kajala Masanja hayawezi kudumu kwani tabia ya Kajala anahijua vizuri.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya Harmonize kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Kajala ambapo walithibitisha hilo siku ya sikukuu ya wapendanao ‘Valentine Day’.

Niva ameeleza kuwa kwa yeye anavyomjua Kajala huwa hadumu kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume hivyo mahusiano yake na Harmonize anawapa miezi miwili tu.

Pia Niva amesema kuwa wasanii wa Bongo movie wana shobo sana na wasanii wa Bongo Fleva na ndio maana wao wasapoti nyimbo zao kwenye mitandao ila huwezi kumuona msanii wa Bongo Fleva anapost movie ya msanii wa Bongo movie.

LEAVE A REPLY