Nini akanusha vikali kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego

0
284

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nini amefunguka na kusema kwamba hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kwa wakati wowote toka wajuane.

Nini amefunguka hayo baada ya kutuhumiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo nyota wa Bongo Fleva baada ya kuonekana wakiwa pamoja.

Baada ya taarifa za kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego kusambaa zilisababisha mwanamuziki huyo kufukuzwa na menejimenti yake ya hapo awali ya Mj Records chini ya producer, Daxo Chali.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego hata siku moja toka waanze kujuana bali ni rafiki yake wa karibu sana hivyo hawezi kufanya hivyo.

Kwasasa mwanamuziki huyo ameachia wimbo mpya uitwao ‘Niwe Dawa’ aliomshirikisha Nay wa Mitego.

Pia amesema kuwa maamuzi ya kufanya nyimbo na Ney wa Mitego yalikuja baada ya kuingia studio na kupata na siyo vinginevyo.

LEAVE A REPLY