Nikki wa Pili afunguka alivyosomeshwa na Ruge

0
61

Staa wa Bongo Fleva, Nickson Simon maarufu kama Nikki wa Pili amefunguka na kusema kuwa alisomeshwa elimu ya chuo kikuu na Ruge Mutahaba.

Nikki ambaye ni memba wa Kundi la Weusi alisema kuwa, wakati anasoma Shahada ya Uzamivu (PHD) alikutana na Ruge na kumuulizia elimu yake.

“Nilikutana naye akaniuliza hivi unasoma nini chuo kikuu nikamwambia Shahada ya Uzamivu basi akasema kuwa anapenda watu wanaojituma katika kusoma nikaachana naye.

“Siku mbili mbele nashangaa wanakuja watu na kuniambia kuwa wametumwa na Ruge kwa ajili ya kunilipia ada yote,” alisema Nikki.

Ruge Mutahaba alifariki dunia nchini Afrika Kusini na mazishi yake yalifanyika nyumbani kwao Bukoba mkoani Kagera siku ya Jumatatu.

LEAVE A REPLY