Nikki Mbishi amchana Fid Q kisa CD ya albam yake

0
47

Mwanamuziki wa hip hop, Nikki Mbishi amesema kuwa amehuzunishwa na Rapa Fid Q kwa kugawa CD ya albamu yake kwa mtu mwingine wakati alimpatia yeye kwa heshima.

Mbishi amesema kwamba kitendo cha Fid Q kumpatia mtu mwingine CD ambayo yeye alimpatia kimempa ukakasi kidogo  lakini ameona hakuna shida japo yeye amemchukulia poa.

“Sikuelewa maana ya kukupatia copy ya album yangu na wewe ukagawa kwa yule jamaa halafu bure tena kwa mtu ambaye hakuwa hata na interest, ni bora ningebaki na CD yangu, maana nilikupa kwa heshima ila nikaona umeichukulia poa”, amesema Mbishi.

Hata hivyo baada ya Mbishi kuanika kuumizwa kwake hadharan,i Rapa Wakazi amekiri kwamba Fid q ni kweli amemkosea rapa huyo huku akimfafanulia jambo linaloweza kuwa sababu.

“Kutakuwa na sababu kubwa nyuma yake. Labda ulikuwa umemuudhi hapo nyuma, akawa ameshikilia hisia ngumu”, amesema Wakazi.

Pamoja na hayo, Rapa Fid Q, amemjibu Nikki Mbishi kwenye sintofahamu hiyo na kusema kwamba “Yule niliyempa CD ni mdau na anamiliki radio sauzi, nilifanya vile baada ya kumtambulisha kwako na nia yangu (niliitamka huku unaisikia) nilitaka akusikie ili ajue wewe ni mahiri kiasi gani na kama kuna uwezekano wa dili basi akupe ni hayo tu”.

LEAVE A REPLY