Ngoma kuwakosa Simba jumamosi

0
356

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Donald Ngoma hatokuwepo kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba kutokana na kuwa majeruhi.

Ngoma amesema haweza kucheza mchezo huo wa watani wa jadi kutokana na kuwa na majeraha hivyo atakuwa nje ya uwanja.

Pia Ngoma amesema kuwa watu wanaosema kuwa amegoma kucheza siyo wa kweli kwani yeye amekuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira hivyo asipocheza itakuwa ni kama dharau, hivyo anadai sababu kubwa inayofanya ashindwe kucheza ni majeruhi na si kitu kingine.

Kwa upande mwingine Donald Ngoma amewataka mashabiki wa Yanga kutokuwa na wasiwasi yeye kutocheza mchezo wa Jumamosi kwani aanaamini Yanga ina wachezaji wengi wapambanaji.

Simba na Yanga zinatatajiwa kucheza kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara siku ya jumamosi Februari 25 mwaka huu huku mchezo wa kwanza wa watani hao ukimalizika kwa matokeo ya 1-1.

 

 

LEAVE A REPLY