Ngoma kuanza mazoezi wiki hii baada ya kupona majeraha

0
255

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma anategemewa kuanza mazoezi wiki hii baada ya kudaiwa kupona majeraha.

Yanga kwasasa inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.

Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh, alimwambia mwandishi wetu kuwa taarifa alizonazo juu ya mshambuliaji huyo ni kuwa anaendelea kupona na hivi karibuni atarejea uwanjani.

Alisema amewasiliana na mchezaji huyo na kumhakikishia kuwa taratibu ameanza kupona na anatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alikaririwa akisema kuwa wanafikiria kuuvunja mkataba na nyota huyo kwa kuwa amekuwa na majeraha ya muda mrefu.

Katika hatua nyingine, Yanga imepanga kuelekea Shelisheli mapema zaidi kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya St Louis ya nchini humo.

LEAVE A REPLY