Neymar ‘hati hati’ kuwakosa Real Madrid baada ya kuumia

0
177

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St Germain, Neymar Junior amehumia na huenda akakosa mchezo wa klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Neymar aliteguka kifundo cha mguu wa kulia kunako dakika ya 76 ya mchezo na kutoka nje huku akibubujikwa na machozi.

Neymar baada ya kuumia jana kwenye mechi dhidi ya Marsely
Neymar baada ya kuumia jana kwenye mechi dhidi ya Marseille

Bado taarifa zaidi za kitabibu hazijatoka kutoka klabu hapo lakini huenda akakaa nje kuanzia wiki tatu, mwezi mmoja na kuendelea.

Kwa hesabu hizo Neymar ana asilimia 60 kuukosa mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Machi 6 mwaka huu.

LEAVE A REPLY