Neymar asikitishwa PSG kutolewa michuano ya UEFA

0
257

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar Jr ameeleza masikitiko yake baada ya kukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid huku akishuhudia timu yake ikitupwa nje ya mashindano.

Neymar ambaye amefanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia alikuwa nyumbani kwao Brazil akifuatilia mchezo huo ambapo PSG imekubali kichapo cha mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo wakiwa nyumbani kwao Parc des Princess.

Baada ya mchezo Neymar alitumia ukurasa wake wa Twitter kueleza hisia zake ambapo ameandika ”Nina huzuni tumeshindwa na huzuni zaidi sikuwa uwanjani kujaribu kuisaidia timu yangu”.

Hata hivyo Neymar aliwapongeza wachezaji wenzake kwa jitihada walioonesha kwenye mchezo huo ambao mabao mawili ya Cristiano Ronaldo na Casemiro yalitosha kuipeleka Real Madrid Robo fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-2.

Katika mchezo wa jana bao la PSG lilifungwa na Endison Cavan huku vinara hao wa Ligue 1, wakimaliza 10 uwanjani baada ya kiungo wao Marco Verratti kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 66.

LEAVE A REPLY