Neverland Ranch ya Michael Jackson yawekwa sokoni

0
176

Nyumba ya kifahari ya Michael Jackson iliyopo Calfornia nchini Marekani “Neverland Ranch” imewekwa sokoni kwa mara nyingine.

Nyumba ya staa huyo imerudishwa sokoni kwa bei rahisi, Neverland Ranch kwa sasa nyumba hiyo la kifahari inauzwa kwa dola milioni 31 wakati mwaka 2015 miaka minne nyuma iliwekwa sokoni kwa bei ya dola milioni 100 lakini haikupata mteja.

Sababu kuu ya nyumba hiyo ya kifahari kuuzwa na familia ya Michael Jackson kwasababu hawana pesa za kuitunza nyumba hiyo.

Neverland Ranch zamani ilijulikana kama Zaca Laderas Ranch na sasa utahitaji dola milioni 31 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 72 ili kulimiki nyumba hiyo.

Nyumba hiyo ndiyo aliyokuwa anaishi Michael Jacksoni enzi za uhai wake kabla ajafariki dunia mwaka 2009 nchini Marekani.

LEAVE A REPLY