Nedy Music atajwa tuzo za Ghana

0
39

Wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nedy Music ‘Ameen’ umetajwa kuwania tuzo za nchini Ghana katika vipengele vitatu ambavyo ni (Global Rec Of The Year,Song Writer Of The Year,Global Male Vocalist).”

Kupitia ukurasa wake wa Instagrm mwanamuziki huyo ameandika shukrani zake

Ameen Nakumbuka Kipindi Ambacho Unafanyika Huu Wimbo Wa Amen, Chini Ya Producer Aloneym Nia Na dhumuni Ilikua, Moja Kuzungumza Maisha Yangu Ambayo Nimepitia Pili Kuwapa Moyo Vijana Kutokata Tamaa, Na wanaoaminishwa Ndoto Zao Na Watu Wengine, Wanaowekewa Vikwazo Katika Malengo Yao, Pia Hata Wanaotegemewa Na Familia Zao Lakini Bado Kipato Kwenye Maisha Yao Ni Kigumu Juu Ya Changamoto Nyingi Sana.

Ukweli Wa Mungu Nakumbuka Niliwahi Kukaa Nyumbani Nikiwa Na Mawazo Mawili; Moja Lilikua Wimbo Utafanya Vizuri Sana Kwa Yale Ambayo Nmezungumza Mule Ndani, Na Lengo Langu Kuwafika Watu Wengi Na Kuwapa Moyo Kwa Tungo Ambazo Zitakua Msukumo Kwao.

Pili; Hofu Ilinijaa Kusema Mziki Wa Kwetu Umekuwa Wa Kubadilika Sana, Na Hasa Watu Waliowengi Hupendezwa Na Kusikia Tungo Za Mapenzi Na Zingine Ambazo Haziusiani Kabisa Na Tungo Kama Za Wimbo Wa  Ameen.

Kipindi Wimbo Unapangwa Kutoka “Tarehe”Ndipo Kipindi Janga La Corona (COVID-19) Limetawala Duniani Kote. Mitandao, Radio & Television Lakini Pia Kila Stori Ya Mtaa.

Leo Mungu Ameonyesha Miujiza Juu Ya Wimbo Huu Kupenya Nje Ya Tanzania. (West) Ghana Kuwa Nominated Vipengele Vitatu Tuzo Za @gmaa.21 Asante Mungu Asante Fine Boy Music Asante Mashabiki  Hakika Kizuri Kitafika Hata Kwa Masiku Yaliyo Na Kiza Dua Thanks For Recognize Me.

LEAVE A REPLY