Nec akijia juu kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

0
115

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekitaka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kutoa uthibitisho wa madai yake dhidi ya NEC na ikishindwa iombe radhi.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima imesema kuwa Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Paul Mikongoti alitoa tuhuma dhidi ya NEC kuhusu matukio yanayohusiana na uchaguzi mdogo katika jimbo la Kinondoni na Siha pamoja na Kata nane za Tanzania Bara.

Kailima amezitaja tuhuma hizo kuwa ni pamoja na kituo cha Televisheni cha ITV kiliadhibiwa na kutakiwa kuomba radhi kwa kurusha habari za kuibiwa sanduku la kupigia kura, Mashirika mabalimbali ya waangalizi kunyimwa vibali vya uangalizi katika uchaguzi huo.

“Baada ya kusikiliza na kutafakari tuhuma hizo dhidi yetu zilizotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, tunapenda kumtaarifu kuwa hakuna shutuma hata moja ambayo ni kweli, ni shutuma dhaifu zisizo na ukweli, hivyo tunamtaka athibitishe na akishindwa aombe radhi mbele ya vyombo vya habari. 

Hata hivyo, ameongeza kuwa NEC inamtaka aorodheshe mashirika yaliyoomba kibali na kijibiwa kama alivyodai na kama hakuna ushahidi huo aombe radhi hadharani.

LEAVE A REPLY