Ndugu wamkaushia Zamaradi baada ya ndoa

0
215

Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi Mketema ameingia kwenye mgogoro na ndugu zake baada ya kushindwa kuwaalika kwenye harusi yake.

Mmoja wa ndugu wa karibu wa Zamaradi amesema ndugu wa upande wa baba yake hawako naye vizuri kwani wanadai hawakushirikishwa wala kualikwa katika shughuli hiyo, kitendo ambacho kiliwakasirisha.

Lakini Zamaradi alipoulizwa kuhusiana na hilo alisema; “Hakuna kitu kama hicho, kwani waliokuwa ndugu zangu wote niliwaalika na walihudhuria kwenye ndoa yangu.”

Hayo yameibuka baada ya hivi karibuni mtangazaji huyo kufunga ndoa na kuzua gumzo jijini baada ya ndoa hiyo.

LEAVE A REPLY