Ndoto ya Riyama ilikuwa kuimba kabla ya kuigiza

0
20

Muigizaji wa Bongo Movie, Riyama Ally amesema kuwa ndoto yake kubwa wakati anakuwa alikuwa anapenda kuimba lakini mambo yakaja kubadilika na kujikuta anaingia kwenye uigizaji.

 

Riyama amesema kwamba baada ya kuona kwamba yeye ndio anaupenda muziki lakini muziki haumpendi yeye ndipo alipoamua kugeuza gia na kujikuta akiwa msanii mzuri wa filamu.

 

Riyama amesema kuwa “Nilikuwa napenda sana kuimba, yaani popote utakaponikuta nilikuwa naimba nyimbo za Khadija Kopa wakati nipo msichana mdogo”.

Pia amesema kuwa siku nikaona kama najilazimisha kufanya hivyo maana hata kucheza nilikuwa siwezi, lakini kuna kipindi nikaja kukutana na watu ambao wakaniingiza kwenye filamu nikafanya poa na ndio mpaka leo naendelea kuzifanya,.

Riyama Ally alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuigiza kwenye filamu ya fungu la kukosa na kuanza kufahamika kutokana na ubora wa uigizaji wake.

LEAVE A REPLY