Ndemla kuelekea Sweden kwa majaribio

0
154

Mchezaji wa Simba, Said Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Sweden kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna.

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Ndemla atakuwa Sweden kwa wiki mbili kujaribu bahati yake katika timu hiyo ya Ligi Kuu ya nchini humo maarufu kama Superettan.

Kama mchezaj huyo mwenye umri wa miaka 21 atafanikiwa  ataungana Thomas Ulimwengu, ambaye  kwa sasa ni majeruhi anasumbuliwa na maumivu ya goti tangu Septemba, mwaka huu na atakuwa nje hadi Januari mwakani.

LEAVE A REPLY