Ndege ya kijeshi ya India yapotea angani

0
152

Jeshi la anga la India (IAF) limethibitisha kupotea kwa ndege ya jeshi lake ikiwa imebeba abiria 20.

Ndege hiyo ya kubebea silaha na mizigo mikubwa, Antonov-32 ilipaa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Chennai (Madras) saa 2:30 kwa saa za India ikiwa inaelekea Port Blair mashariki mwa visiwa vya Andaman na Nicobar.

Ndege hiyo ilipangwa kutua saa 5:30. Tayari msako mkali wa kuitafuta umeshaanza ukihusisha vyombo mbalimbali zikiwemo meli na ndege nyingine.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba wataalamu waliokuwa wanapelekwa kwenya kisiwa muhimu karibu na Malaka Straits ambapo kuna kambi ya jeshi la India.

LEAVE A REPLY