NBA kufungua chuo cha Basketball Senegali

0
131

Chama cha mpira wa kikapu cha Marekani (NBA) kinaanzaa mkakati wa kufungua chuo cha kujifunza mchezo huo barani Afrika ili kukuza vipaji zaidi vitakavyopelekwa kujiunga na timu za Marekani.

Chuo hicho kinachotarajiw akufunguliwa mwakani kinatajwa kujengwa kwenye mji wa Thies nchini Senegali kufuatia hatua kama hiyo iliyofanywa kwenye nchi za Australia na China.

Chuo hicho kinatarajia kuwachukua wanafunzi wenye vipaji vikubwa zaidi vya mchezo huo wenye umri wa kuanzia miaka 13.

Mkurugenzi wa NBA barani Afrika, Amadou Gallo Fall ameliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa majaribia ya mwanzo yameshafanyika nchini Senegali.

LEAVE A REPLY