Nay wa Mitego: Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa

0
331

Mwanamuziki wa hip hop nchini, Nay wa Mitego amesema kuwa usalama wa maisha yake umekuwa mdogo kwasasa.

Nay ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kueleza hali ya maisha yake kwasasa toka atoke mahabusu alipokamatawa kutokana na kuimba wimbo ‘Wapo’ uliodaiwa kuikashifu Serikali iliyopo madarakani.

Kupitia akaunti yake Instagram Nay wa Mitego ameadika kama ifuatavyo.

“Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine.”

Aliongeza kwa kuandika Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod.

LEAVE A REPLY