Nay wa Mitego kuachia albam mpya

0
72

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Nay wa Mitego ametangaza kuwa kwa sasa anaandaa Album yake mpya ambayo imefikia nusu ya maandalizi.

Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki, alitoa taarifa hiyo kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii leo Septemba 19 2021.

Nay kwenye taarifa yake hiyo aliongeza kuwa kuazia sasa nyimbo atakazoachia zitakuwa ni kutoka kwenye ujio wake huo wa Album.

Mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuingojea albam yake hiyo mpya ambayo inakaribia kukamilika kwasasa.

LEAVE A REPLY