Nay wa Mitego azikwepa skendo mwaka huu

0
313

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amesema kwa sasa hataki tena kusikia mambo ya skendo zaidi ya kufanya kazi yake ya muziki.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa skendo ya mwanamuziki huyo kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake anayefahamika kama Nini.

Nay wa Mitego amesema kuwa mwaka huu anahitaji kutoa ngoma kali siyo mambo ya skendo kwasababu mziki wa sasa umebadilika.

Amesema Nay “Huu sio mwaka wa kupigishana na watu kelele ni kazi tu ndio zinakuwa zinaongea, hata kwa wewe mtangazaji ukisikia skendo hata usinipigie simu, so huu ni mwaka wa roho mbaya, panapo majaaliwa next week tutaonyesha huu ni mwaka wa roho mbaya.

Nay kwa sasa kumekuwepo na stori kuwa Nini na Nay wa Mitego wapo katika mahusiano ya kimapenzi tangu kutoa ngoma yao iitwayo Niwe Dawa ingawa wote wawili hukanusha pindi wanapoulizwa.

LEAVE A REPLY