Nay wa Mitego apigiwa simu na vingozi kisa wimbo wake mpya ‘Alisema’

0
111

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amesema kuwa amepokea simu kutoka kwa baadhi ya viongozi nchini wakimpongeza kutokana na wimbo wake mpya ‘Alisema’.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Nay wa Mitego amesema kuwa kwake ameshangazwa sana na kitendo cha viongozi hao kwani si kawaida kufanya hivyo.

Nay wa Mitego ameachia wimbo huo siku Oktoba 6 mwaka huu ambapo ndani ya wimbo huo amezungumzia masuala mbali mbali ya siasa, uchumi, na maendeleo ya nchi pamoja na hali maisha ya wananchi kwa ujumla.

Nay wa Mitego leo amedai kuwa Viongozi wengi nchini wameonekana kumshangaza, baada ya kumpigia simu na kumpa pongezi nyingi kutokana na ngoma yake mpya ya “Alisema” aliyoiachia rasmi October 6,2018.

Nay Wa Mitego amesema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa viongozi tofauti tokea aachie ngoma hiyo, kitu ambacho kinamshangaza na kumpa maswali mengi.

Nay amedai kuwa kuwa ni kitu gani vingozi wamekipenda kwenye ngoma yake ya ‘Alisema’ mpaka kumpa pongezi hizo.

LEAVE A REPLY