Nay wa Mitego amjia juu Babu Tale kuhusu Zari

0
430

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha.

Pia amesema “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

LEAVE A REPLY