Nay wa Mitego akatazwa kuimba na mama yake

0
299

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa mama yake mzazi hataki aendelee kuimba nyimbo zinazohusu masuala ya siasa.

Nay amesema kuwa Mama yake hataki afanye muziki kwa sababu ya matatizo anayokutana nayo katika kazi zake za uimbaji.

Nay amesema kuwa sababu mara ya mwisho alipokamatwa baada ya kutoa Wimbo wa Wapo ndiyo alimkataza kuimba na afanye shughuli nyingine mana atakuja kufa siku si zake.

Kuhusu wimbo wake mpya ‘Alisema’ Nay amedai kuwa wimbo huyo ameufanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na mashabiki wa muziki wake na amefanya kwa ajili ya hali iliyopo kwa sasa nchini.

Naya amesema kuwa  “Ninampenda sana mama yangu na huwa ninamsikiliza sana, lakini kwa Wimbo wa Alisema nilijua tu unaweza kuzua balaa (utata), lakini nilipokuwa nikiendelea na kukumbuka kauli ya mama wakati nimeingia studio na kurekodi ndiyo nikaambiwa hebu weka sawa mashairi yako na ndipo nikayapangilia na wimbo ukatoka kama mnavyousikia.

“Siyo kwamba sitafanya muziki, kuna dizaini ya muziki ambayo mama yangu hataki kusikia nikifanya hasa nyimbo za harakati kama hizi huwa hapendi kabisa kusikia. Kwenye muziki nitaendelea, lakini kwa nyimbo hizi za harakati ambazo mama yangu hazitaki sitafanya kabisa”.

LEAVE A REPLY