Nay wa Mitego akataa kujihusisha na siasa

0
96

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa hawezi kujihusisha na siasa wala kugombea ubunge kwasababu siasa ya Tanzania imejaa uongo.

Nay wa Mitego ameongea kauli hiyo baada ya siku kuenea habari kuwa msanii uenda akajiingiza kwenye siasa kutokana na baadhi ya nyimbo zake kuikosoa serikali lakini mwenyewe amepinga vikali suala hilo.

mitego amekataa swala hilo huku akisema kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu anaona kabisa kuwa yeye hawezi siasa ya Tanzania.

Nay wa Mitego anasema kuwa kugombea ubunge hatoweza kwa sababu siasa ya tanzania imejaa uongo mwingi sana na hana haja ya kukaa na kudanganya wananchi wake pia.

Pia amesema kuwa amekuwa na ndoto ya kuwa rais lakini rais asiyekuwa na mambo mengi zaidi ya kufanya vitendo tu na kunyoosha mambo kama anavyofanya sasa katika Sanaa.

LEAVE A REPLY