Nay wa Mitego adai BASATA wanashusha muziki

0
139

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka na kusema Muziki wa Bongo fleva uko mbioni kupotea kama ilivyo Bongo Movie kutokana na sharia za serikali na BASATA.

Wiki chache zilizopita Nay wa Mitego alikuwa mmoja kati ya wasanii waliofungiwa nyimbo kuchezwa kwenye vyombo vya habari kwa madai kuwa haziendani na maadili ya Tanzania.

Maoni hayo ya Nay wa Mitego  yalikuja baada mjadala mzito kati ya Naibu Waziri wa habari Juliana Shonza na viongozi wa BASATA walipokuwa wanajibu maswali mbali mbali kuhusu hatua wanazoendeela kuchukua dhidi ya wasanii hao.

Kwenye mjadala watu wengi waliuliza maswali kuhusiana na vigezo vya kufungiwa kwa wasanii na nyimbo zao huku wengine wakihoji kwanini BASATA wanasimamia kigezo cha maadili pekee? lakini majibu kutoka BASATA hayakuwaridhisha wala kuwaingia vichwani baadhi ya wasanii akiwemo Nay Wa Mitego.

Nay wa Mitego alitumia ukurasa wake wa Twitter na kuweka ujumbe wake huo wa kukata tamaa juu ya Bongo fleva.

LEAVE A REPLY