Nay afunguka sababu ya kuitwa Basata

0
77

Mwanamuziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amefunguka sababu ya kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) siku ya jana Jumatatu.

Nay aliwasili katika ofisi za Baraza hilo kwa ajili ya kusikilza wito alioitiwa jana na kusababisha taharuki dhidi yake kutokana na wito huo.

Nay amesema kuwa alipewa barua na baadhi ya kiongozi wa Baraza hilo kufika ofisini kwa ajili ya mazungumzo huku Nay akidhani wito huo utakuwa kwa ajili ya wimbo wake mpya “Alisema” ambao ndani unazungumzia masuala ya Serikali.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa alidhani barua hiyo itakuwa inahusu wimbo wake mpya ‘Alisema’ ambao ameuachia siku chache zilizopita.

Pia Nay amesema kweli baada ya kupokea simu ya BASATA aliishiwa nguvu kabisa lakini baada ya kufika eneo la tukio akakuta ni barua kuifungua kumbe ni ishu za kazi tu.

LEAVE A REPLY