Navy Kenzo wafunguka kuhusu kubuma kwa wimbo wao ‘Fela’

0
928
Aika na Nahreal

Wasanii kutoka kundi la Muziki la Navykenzo Nahreel na Aikah Marealle wamekana maneno maneno yanayosemwa dhidi ya single yao mpya inayoitwa ‘Fela’ kudaiwa kubuma.

Navykenzo walitoa Fela siku chache zilizopita lakini kuna tetesi kuwapatanisha wimbo huo umebuma kwani haujapata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki.

Aika ameweka wazi kuwa wimbo wao mpya wa Fella, haujabuma bali unafanya vizuri na kipimo cha wimbo kufanya vizuri kwao si ‘views’ za Mtandao wa YouTube pekee.

Navykenzo ambao wamekuwa na kawaida ya kutoa nyimbo ambazo siku zote zimekuwa zikifanyavizuri kama vile Kamatia chini na game na nyinginezo wamesisitiza na Fela ipo kwenye kundi hilo.

LEAVE A REPLY