Navy Kenzo kuja na albam mpya

0
58

Kundi la muziki wa Bongo Fleva linaloundwa na wasanii wawili ambao ni Nahreel na Aika, Navy Kenzo wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya.

Wamekuwa  kimya kwa muda huku wakiachia kazi moja moja bila mashabiki wao kujua mipango yao kimuziki imekaaje.

Awali ilitakiwa watoe EP Project lakini kila wakikaa na kupitia stock yao ya nyimbo wakajikuta inawawia vigumu kufanya maamuzi ya kukamilisha EP hiyo na kuwapa mashabiki project yenye nyimbo chache.

Haijawekwa wazi project hiyo itakuwa na nyimbo ngapi au itaitwaje, ila watu walio karibu na kundi hilo wanasema ni project ambayo itakidhi kiu ya muziki wa Navy Kenzo uliokosekana kwa muda kidogo.

Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mambo mengi mazuri kwa Navy Kenzo, waliachia nyimbo kadhaa ikiwemo: FELLA yenye views zaidi ya 1,800,000 kwenye mtandao wa YouTube, MAGICAL yenye views zaidi ya 350,000 na ROLL IT yenye views zaidi ya 350,000.

LEAVE A REPLY