Nape awakutanisha Diamond na Alikiba kwenye kamati ya Serengeti Boys

0
425

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amewakutanisha Alikiba na Diamond kwenye kamati ya watu 10 kwa ajili ya kuhakiksha Serengeti Boys inafanya vizuri kwenye mashindano ya Afcon nchini Gabon.

Nape ameamua kuwaweka wanamuziki hao kwenye kamati hiyo kutokana na uwezo wao wa kuhamasisha wanamichezo kuisapoti timu hiyo kwasababu wanamashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Alikiba na Diamond ni wanamuziki wanaofanya vizuri kwasasa na hawana mahusiano mazuri baina yao kutokana na uhasama kwenye kazi zao za muziki.

Kamati hiyo inaundwa na watu 10 ambapo mwenyekiti wake ni Charles Hillary na wengine ni Celesitne Mwesigwa, Beatrice Singano, Maulid Kitenge, Ruge Mutahaba na Eric Shigongo.

Pia Waziri Nape amewataka pia wadau wa soka na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuiunga mkono Serengeti Boys katika mashindano ya Afrika nchini Gabon ili ifanye vizuri na kuwa kama sehemu ya mtaji wa kwenda Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.

 

 

LEAVE A REPLY