Nape amewataka waliojenga maeneo ya michezo kuachia maeneo hayo

0
135

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka wananchi waliojenga maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya Viwanja vya Michezo kuhakikisha wanayaachia ili yaweze kutumika kama ilivyopangwa.

Nape amesema wameshaandaa Program maalum ambayo itahusika na kufuatilia watu waliyojenga maeneo ya wazi ambayo yametengwa maalum kwa ajili ya viwanja vya Michezo ili kuhakikisha kunakuwa na viwanja vingi ambavyo vitawasaidia watoto kuweza kupata maeneo ya kuendeleza vipaji vyao.

Waziri huyo amesema kuwa anaamini maeneo ya wazi yaliyovamiwa yapo mengi na jitihada za kuyarudisha zitafanyika kama ilivyoahidiwa ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na maeneo ya karibu ya kufanyia mazoezi na hata watoto pia wanapata viwanja kwa ajili ya michezo.

Pia Nape amesema kwasasa serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo nchini inajipanga kuhakikisha ushiriki wa wanamichezo wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2020 nchini Japan unaongezeka ili kuongeza uwezekano wa kufanya vizuri katika mashindano hayo.

LEAVE A REPLY