Nape ameunda Kamati kuchunguza sakata la Makonda kuvamia Clouds Media

0
385

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza tuhuma kuhusu tukio la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media.

Nape amesema hayo leo akiongea na waandishi wa habari alipotembelea ofisi za Clouds Media ambazo zilivamiwa na mkuu wa mkoa huyo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape amesema kuwa ripoti itakayopatika kutoka kwenye kamati hiyo itatangazwa baada ya masaa 24 na akitofichwa kitu kuhusu taarifa hiyo ambayo inawatia mashaka waandishi wa habari.

Nape amewataka watanzania na waandishi wa habari kwa ujumla kuwa watulivu wakiisubili ripoti hiyo ndani ya masaa 24.

Pia Nape amesema kuwa baada ya ripoti hiyo kukamilika hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mkuu wa mkoa huyo zitatangazwa hadharani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa IPP Media, Reginard Mengi amesema kuwa kitendo hiko si kizuri kabisa na amemuomba waziri Nape kulichukulia hatua suala hilo kutokana na kuingiliwa kwa tasnia ya habari.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anashtumiwa kuvamia studio za Clouds Media akiwa na askari wenye silaha kali baada ya Clouds TV kukataa kurusha kipindi chenye tuhuma za Gwajima.

 

LEAVE A REPLY