Nandy kuvalishwa pete nyingine na Billnass

0
38

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kusema kuwa anatarajiwa kuvishwa pete ya uchumba kwa mara ya pili baada ya awali kuibiwa.

Nandy alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Billnass, Aprili mwaka jana katika shoo ya Homa inayorushwa na kituo cha Tv cha TVE.

Nandy amesema pete ile ya awali iliibwa na vibaka akiwa kwenye shoo mjini Tanga, mwaka jana ndio maana analazimika kuvishwa nyingine, ila na Billnass huyohuyo.

Nandy alifafanua pia kuwa kuvalishwa pete hiyo nyingine kwa sasa hana uhakika sana, kwani hata uvalishwaji wa pete ya kwanza wazazi wake hawakuibariki.

Pia amesema kuwa hajui lini atavalishwa pete hiyo kwani jambo hilo amemuachia Billnass kwa kuwa yeye ni mwanaume, na ndiye mwenye kupanga hilo.

LEAVE A REPLY