Nandy kuja na tamasha lake 2021

0
135

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameweka wazi kuwa anatarajia kuja na Festival yake itakayoitwa Nandy Festival itakayofanyika mikoa tofauti hapa nchini.

Nandy amesema kuwa ifikapo mwaka 2021 kutakuwa na Nandy festival na imeshaplan-iwa mapema sana na watu tutakao kuwa tunashirikiana nao, unajua hivi vitu haukurupuki.” Ameeleza mrembo huyo kupitia Rick Media.

Pia akaongeza “Awali nilikuwa nafanya mimi mwenyewe bila sapoti kutoka sehemu yoyote kuanzia wasanii na kila kitu lakini nashukuru mungu.

Nimefanya kitu kimeonekana sasa nawaomba watu waingize mkono wao, na itakuwepo tena mapema sana mwakani hivyo watu wakae tayari kwa tamasha hilo.

LEAVE A REPLY