Nandy avunja ukimya, afunguka ishu ya Ukimwi

0
107

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa watu waache kumuuliza kuhusu kudaiwa kuwa na ugonjwa wa Ukimwi kwani anajisikia vibaya katika jamii.

Nandy amesema kuwa kama wataendelea kumpakazia kuhusu ugonjwa huo kwasababu itawafanya wale wanaoumwa kweli ugonjwa huo wajione sio binaadam wa kawaida.

Akitoa taarifa hiyo kwenye ‘Insta Story’ yake ya mtandao wa Instagram Nandy ameandika kwa masikitiko.

Ameanza kwa kuandika “Swali la Ukimwi pia muache kuniuliza otherwise unataka nikupunguzie kidogo na tuheshimiane, mnafanya hata wale wanaoumwa kweli wajione sio binaadam wa kawaida hofu ya Mungu itawale”.

Aidha Nandy ametoa taarifa nyingine ambayo inadhibitisha kuachana na Billnass ambapo anasema hataki kuulizwa kuhusu mahusiano tena na wampe muda wa miaka mitana tena.

LEAVE A REPLY