Nandy aomba radhi baada ya video yake chafu akiwa na Bilnass kusambaa mtandaoni

0
612

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ameomba radhi baada ya video yake chafu akiwa na Bilnass kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Video hiyo imezua gumzo leo katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha wawili hao wakiwa faragha kitandani jambo ambalo limewakera mashabiki wa mwanamuziki huyo huku akikiri kuwa video hiyo ni kweli japokuwa ni yam waka 2016.

Nandy amesema kuwa video hiyo imechukuliwa akiwa katika uhusiano na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Bilnass ambapo walikubaliana kuwa ya siri.

Nandy ameendelea kusema kuwa hajua Bilnass ana maana gani mpaka kupelekea kuvujisha video hiyo katika mitandao ya kijamii.

Amesema kuwa “Nawaomba radhi kwa mashabiki wangu, familia yangu, kanisani kwangu na serikali.  Kiukweli video imenichafua sana ila adhabu ya maumivu haya ninayoyapata sasa hivi ni kutokana na kumuamini Billnas.

LEAVE A REPLY