Nandy akanusha kuwa mjamzito

0
47

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amekanusha tetesi kuwa ana ujauzito baada ya kuonekana ana kula udongo katika baadhi ya video zake katika mtandao wa Snapchat.

Nandy ameamua kuweka wazi suala hilo kutokana na madai ya kuwa na ujauzito wa Billnass baada ya kuonekana kula udongo kwenye mtandao wa Snapchat siku kadhaa zilizopita.

Nandy amesema watu wanamsema ni mjamzito kwa sababu ya ongezeko la mabadiliko yake ya mwili wake ambayo yanasababishwa na ukuaji.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wangu ambayo yanasababisha kukua haraka kama kunenepa.

Billnass na Nandy tayari wameshavalishana pete ya uchumba na kinachosuburiwa kwa wawili hao kwasasa ni ndoa kwa wasanii hao.

LEAVE A REPLY