Nandy akanusha kugombana na Wema Sepetu

0
43

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amesema kuwa hajawahi kugombana na msanii mwenzake Wema Sepetu na wala hajawahi kumchukulia bwana kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea.

Nandy amesema kwamba kipindi cha nyuma, kuna maneno mengi yalisambaa mitandaoni kwamba yeye na Wema ni kama chui na paka kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wameibiana mabwana, jambo ambalo halina ukweli.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Mimi na Wema hatujawahi kugombana kabisa, nilikuwa nashangaa wanavyosema eti nilimuibia danga lake kitu ambacho hakina ukweli wowote, siwezi kufanya hivyo’.

Nandy ameongeza kwa kusema kuwa Watu huwa wanaongea sana halafu wanaongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo, nampenda Wema na sitaacha kufanya hivyo, zaidi tunasapotiana sana kwenye kazi.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo Acha Lizame aliomshirikisha mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Harmonize.

LEAVE A REPLY