Nandy ahairisha ziara yake nchini Marekani

0
279

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ametangaza kuahirisha ziara yake ya kimuziki nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Kuahirishwa kwa ziara yake hiyo nchini Marekani  kumetokana na athari za Ugonjwa wa Corona ambao unautikisa dunia na kupelekea miji mbalimbali kufungwa duniani kutokana maambukizi kuwa makubwa nchini humo.

Nandy alipaswa kuanza ziara yake hiyo mnamo March 22,2020 ambapo angeanza Columbus na kuihitimisha June 27, 2020 Jijini Washington nchini Marekani.

Pamoja na kuahirisha ziara hiyo Nandy amewajuza mashabiki wake walionunua tiketi kuwa wasiwe na hofu kwani tiketi hizo zitatumia pale watakapotangaza tena kufanyika kwa ziara hiyo.

Ugonjwa wa Corona umekuwa na atahri kubwa duniani kote hususani nchini Marekani ambapo watu zaidi ya elfu 55 kufariki kutokana na ugonjwa huo ulioanzia nchini China.

Nandy anakuwa mwanamuziki wa pili nchini kuahirisha ziara yake nchini Marekani baada ya Diamond kufanya hivyo mapema kutokana ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY