Nandy afuata nyayo za Harmonize

0
553

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nandy ameachia video ya wimbo mpya unaoitwa kwa jina ‘Magufuli Tena’ ambao umempongeza Rais John Pombe Magufuli.

Wimbo huo unaoelezea kwa kina hatua za maendeleo ya Tanzania na uchapakazi wa Rais Magufuli, video inaonesha Maendeleo yaliyofikiwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya Madaraka.

Wimbo huo wa ‘Magufuli Tena’ ni marudio ya Melody na Mdundo wa wimbo wake uliofanya vizuri wa ‘Ninongeshe’ uliotoka 2018.

Nandy anakuwa mwanamuziki wa pili kuimba wimbo kusifia utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli baada ya Harmonize kufanya hivyo kwenye wimbo wake uitwao Magufuli.

Nyimbo hizo zinaongelea mambo mbali mbali yaliyofanywa na Rais Magufuli katika serikali yake ya awamu ya tano kama vile ununuzi wa ndge, Ujenzi wa reli mpya, pamoja ujenzi wa barabara.

LEAVE A REPLY